HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 3 Mei 2018

Caf Kuichezesha Yanga Usiku Dar


Wachezaji wa Yanga wakifanya mazoezi.

HUKU mashabiki wakihofia miundombinu ya umeme na hali ya hewa ya Dar es Salaam, CAF imepanga mechi ya Yanga na Rayon ichezwe Mei 16, Saa 1 usiku.

Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatano na CAF hupanga ratiba hiyo kutokana na haki za televisheni ambazo wanamiliki wao lakini hata klabu mwenyeji huruhusiwa kutoa maoni.

Kwa mujibu wa CAF mechi za Kombe la Shirikisho zitachezwa mara mbili kwa wiki ambapo moja itapigwa Jumatano na nyingine Jumapili. Jumamosi hakutachezwa mechi yoyote ya Shirikisho zaidi ya Ligi ya Mabingwa.

Hiyo itakuwa ni mechi ya kwanza ya Yanga kuchezwa usiku katika siku za hivi karibuni kwani nyingi zimekuwa zikichezwa mchana kutokana na miundombinu ya Dar es Salaam haswa kwenye suala la umeme.

Msemaji wa Yanga, Dismas Ten ameliambia Championi Jumatano kwamba wameridhia muda huo ili kuruhusu mashabiki wengi waone mchezo huo na hawaihofii Rayon kwa vile wanaimudu.

Mechi ya Simba na Al Masry ya Kombe la Shirikisho ilipigwa usiku kwenye Uwanja wa Taifa umeme ukakatika na kuzua tafrani sambamba na mvua.