HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 9 Novemba 2017

MAPYA YAIBUKA NDOA YA DOGO JANJA NA UWOYA WEMA AHUSISHWA

Mapya Yaibuka Ndoa ya Dogo Janja, Irene Uwoya Wema Ahusishwa





Nyuma ya sarakasi ya kile kinachosemekana ni ndoa kati ya staa wa Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya na dogo wa Bongo Fleva, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kuna mengi, Amani limeibuka na jipya. DILI LA MIL.
400 LA WEMA Ilifahamika kuwa, dili hilo lilikuwa liende kwa Wema Isaac Sepetu ambaye miezi kadhaa aliripotiwa na gazeti ndugu la hili, Ijumaa Wikienda kuwa alikuwa amelamba shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuandaa tamthiliya hiyo.
    Ilidaiwa kwamba, baada ya sakata la Uwoya na Dogo Janja likishika kasi ndipo kukaibuka ubuyu kwamba, dili hilo aliporwa Wema la sivyo ndiye angeolewa na Dogo Janja ndani ya tamthiliya hiyo.
   “Wema alihakikishiwa kabisa kushikishwa shilingi milioni 400 na akaanza kufanya usaili wa mastaa zaidi ya hamsini atakaowatumia na kuwaahidi kuwalipa dau nono.
  UWOYA ANUKA FEDHA “Lakini ghafla ilidaiwa kwamba, Uwoya alifanya ‘umafia’ ndipo dili likahama kwa Wema na kutua mikononi mwake kisha kukamata huo mkwanja na sasa ananuka fedha maana zimemtembelea bidada.
   “Ilikuwa rahisi kushinda tenda hiyo maana wakati Wema anataka ashikishwe shilingi milioni 400, yeye alidaiwa kukubali kufanya kazi hiyo kwa shilingi milioni 200 na ushee.
   “Unaambiwa sasa hivi bifu la Uwoya na Wema linafukuta na ukizingatia kwamba huwa hawaivi chungu kimoja.
  “Nakwambia inasubiriwa siku watakutana uso kwa uso watu waone itakuwaje maana hawajaonana tangu kutokea kwa ishu hiyo.
  “Unaambiwa Wema ana hasira maana tonge lilimponyoka mdomoni hivyo Team Wema wanamuomba Uwoya akae mbali nao,” kilimaliza kumwaga ubuyu chanzo na kulipisha Amani liwatafute wahusika.
MDHULUMIWA WEMA Jitihada za kumpata Wema ziligonga mwamba baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, lakini alipotafutwa Neema Ndepanya ambaye ni prodyuza na mwandishi wa miswada wa Wema alikuwa na haya ya kusema: “Ni kweli Wema alikuwa na dili kama hilo lakini siwezi kusema ndilo hilo unalolizungumzia (la Uwoya).
   UWOYA ASHTUKA Alipotafuta Uwoya na kuulizwa juu ya kupora dili la Wema alishtuka na kudai kwamba, ndiyo kwanza anasikia ishu hiyo kutoka kwa mwandishi wetu.
  “He! Ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako (mwandishi) na sina maoni juu ya hilo maana sielewi chochote.”
Chanzo: Global Publishers Visit website