HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 6 Aprili 2018

Ajali nyingine yatokea Mbeya, 44 wanusurika kifo

Ajali nyingine yatokea Mbeya, 44 wanusurika kifo


Watu 44 wakiwemo Waandishi wawili wa habari wa kituo cha ITV na TV One Mkoani Mbeya wamenusurika kufa baada ya basi aina ya Mistubishi fuso walilokuwa wakisafiria kutoka Wilayani Chunya kuelekea Jijini Mbeya kupinduka na kuwajeruhi vibaya abiria nane.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 1:45 usiku wa kuamkia leo baada ya basi lenye namba za usajili T647 CAQ Mitsubishi fuso kufeli breki katika mtelemko mkali wa Mwansekwa, eneo la Igodima nje kidogo ya Jiji
la MbeyaÖ.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Jeshi la polisi, Mohamed Mpinga anasema chanzo cha ajali ni ubovu wa gari hilo ambao umesababisha brek zake kufeli

Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dk Goodlove Mbwaji anasema amepokea majeruhi 44 wa ajali hiyo na kudai kuwa kati ya majeruhi hao majeruhi nane walikuwa na hali mbaya hivyo wakalazimika kulazwa hospitalini hapo, huku wengine wakitibiwa na kuruhusiwa