HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 18 Aprili 2018

Aliye nusurika kifo shindano la kunywa pombe ajipanga kuokoka

Asiyejua kufa mwambie achungulie kaburi, ndivyo ilivyotokea kwa Patrick Paulo (26) mkazi wa Morotonga wilayani Serengeti mkoani Mara ambaye amenusurika kifo katika shindano la unywaji pombe kali.

Katika shindano hilo ambalo mgambo Zakayo Thomas (50) maarufu kama Hayaishi, mkazi wa Ngarawani, alikufa papo hapo na kukosa dau la sh 100,000 walilokuwa wanashindania na wanywaji wenzake.

Paulo (pichani) ambaye hiyo ni mara yake ya pili kuingia kwenye mashindano hilo la kunywa pombe ilia pate fedha na kuponea chupuchupu, kwa sasa anaonekana mwenye majuto baada ya kushuhudia mwenzake anakufa.

“Siamini kama nimepona, maana hali ilikuwa mbaya sana, kama kuna kuokoka sasa ndicho kipindi changu cha kumrudia Mungu na inawezekana Mungu ana makusudi yake,” anasema Paul katika hali ya utulivu akionekana kuguswa na tukio hilo ambalo lilimsababishia kifo mshindani mwenzake huku yeye akinusurika.

Aliingiaje kwenye shindano?

Aprili 10 majira ya saa 12 jioni mwaka huu akiwa katika mizunguko yake alipita kwenda Baa ya Fm mjini Mugumu na kukuta shindano la kunywa pombe chupa 10 pamoja na bia mbili, mshindi wa shindano hilo alitengewa kitita cha Sh 100,000.

“Kwa usawa huu nikaona naweza kuibuka mshindi, kama vijana wengine wanabet nami nikaona nijaribu,nilipewa sharti la kwanza kunywa bia mbili,nikaanza nazo kwa kujiamini kisha nikawekewa chupa 10 za pombe,”anasema.

Anasema wakati huo mgambo Thomas ambaye sasa ni marehemu akionekana kuchoka kwa ulevi aliamka taratibu kama anaenda uani lakini ghafla alianguka chini, watu waliokuwa pale wakaanza kumcheka na kumbeza kadri walivyoweza wakidhani ataamka.

“Walidai aachwe apigwe upepo kwanza, wakati mimi nikiwa naendelea kufakamia chupa, ghafla mwenzetu mmoja ambaye alikuwa kiongozi wa wadhamini akaweka Sh100,000 mezani hapo nikahamasika zaidi,” anadai Paulo.

Baada ya kupiga chupa ya tano aliishiwa nguvu na kutoroka, hata hivyo njiani aliishiwa nguvu na kuanguka lakini alipozinduka alijishangaa kujikuta yuko hospitali akiwa amewekewa chupa za maji.

Pambano lake la pili

Paulo anayeishi Mtaa wa Uswazi kwa sasa eneo ambalo ni maarufu kwa uuzaji wa pombe mchanganyiko, anadai kuwa katika pambalo la kwanza nalo alikimbia.

Shindano la kwanza lilikuwa la pombe za kwenye vifuko vya plastiki zilizowekwa kwenye chupa, alishindwa kumaliza chupa 10 baada ya kuzidiwa na angeendelea huenda angekufa huku wadhamini wa mashindano ambao ni wale wale walikuwa wakimdhihaki kwa kuwa sanda ilikuwa imeandaliwa.

Awataka wasaidie vijana

Paulo ambaye amepewa masharti ya kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye kujenga mwili, kulinda na kutia joto anakabiliwa na ukata na anaomba wanaodhamini watu kunywa pombe wasaidie vijana kwenye miradi ya maendeleo.

“Sijui wanapata faida gani zaidi ya kusababisha vifo vya watu, wanakamatwa lakini baadaye wanaachiwa, kuna watu wana matatizo mengi ya kiuchumi lakini wao wanataka kuharibu watu kwa pombe, hili lazima litazamwe vizuri,”anasisitiza.

Anakiri kuwa pombe hizo ni zaidi ya zile zinazowekwa kwenye vifuko vya plastiki ambazo zilipigwa marufuku na Serikali na anasisitiza kwamba kama hatua za haraka hazitachukuliwa madhara yataendelea kuwa makubwa hasa kwa vijana.

Atamani ufundi

Kupitia matukio hayo mawili na alivyoshuhudia mtu anakufa sababu ya pombe sasa anadai akipata mtu wa kumsaidia kujiendeleza zaidi katika ufundi wa magari kwa kuwa ni kazi ambayo amewahi kujifunza.

Wanaweka maji

Mmoja wa wauzaji wa baa (jina limehifadhiwa) anasema kuna mbinu mpya imeibuliwa na vijana wanaoshiriki shindano la kunywa pombe ili waweze kushinda na kuchukua pesa.

“Wanakuja tunachukua chupa tupu za pombe aina mbalimbali kisha tunaziweka maji, tunazifunga na kuzipanga pamoja na nzima, wakifika tunachofanya ni kuzitoa zile za maji na mwisho nzima mbili, mmoja anaposhinda tunagawana kitita,”anasema muuzaji huyo.

Anasema pombe hizo zina nguvu kubwa,” anaitaja pombe moja ambayo chupa yake ina ujazo wa 200 mil na kilevi asilimia 42, kuna nyingine ambayo ujazo wake mil 200 na kiwango cha kilevi ni asilimia 40, hizi ni pombe kali sana na watu wengi wanaofakamia wanaishia pabaya,”anasema.

Ukali wake watisha

Kutokana na ukali wa pombe hizo kumeibuka mtindo wa kugawa mara mbili kwenye chupa,”sasa hivi wauzaji wanachupa tupu ambazo wanatumia kugawa mara mbili pombe hizo na kuuza Sh 1000, hii ni hatari nyingine inayowakabili vijana na wanywaji kwa ujumla,” anasema Joseph Magoiga.

Magoiga ambaye ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Chamoto anasema kwamba ‘uchakachuaji’ huo una madhara makubwa kwa watumiaji kiafya kwa kuwa wanaweka kwenye chupa ambazo zilikwishatumika na haijulikani usafi wake ukoje.

Anasema kuondoa pombe zinazowekwa kwenye vifuko vya plastiki bado hakujasaidia kwa kuwa sasa wameibuka na mtindo huo ili kuwawezesha wateja wale wa pombe zilizokuwa zikiwekwa kwenye vifuko vya plastiki kununua hizi nyingine lakini tatizo ni kwamba ulevi wa sasa ni tofauti na ule wa zile pombe zilizokuwa zikiwekwa kwenye vifuko vya plastiki.

“Kama mamlaka zitaendelea kulala licha ya kujua kinachofanyika vijana wataendelea kupotea na hakutakuwa na nafuu yoyote kati ya wakati ule pombe zikinunuliwa kwenye vifuko vya plastiki na sasa, pia hizi pombe zichunguzwe kali sana,” amesisitiza.

Kifo cha mgambo chastua

Kifo cha Mgambo Thomas kimeibua mjadala kuwa huenda ni mkakati maalum kutokana na kazi zake za mgambo na pia msiri wa Polisi (Infoma) ingawa uchunguzi ulibaini kuwa ni unywaji wa pombe kuzidi kiasi.

Inadaiwa kuwa yeye alipewa bia mbili na kunywa chupa nane za pombe nyingine ambazo ni kali na hivyo kuzidiwa kisha akaanguka na hakupata msaada wowote kwa kuwa wadhamini na mashabiki waliokuwepo walidai ataamka tu.

Gabriel Saimoni Mwenyekiti wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu la Geitasamo anadai kuwa hilo ni tukio la pili kwa kundi hilo la kudhamini watu kunywa pombe na kufariki.

“Hawa wanatakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili sheria ichukue mkondo wake, maana wanawezaje kuendesha michezo yenye kusababisha vifo kama hivyo wakaachwa,”anadai.

Mtaalamu anena

Mmoja wa wataalamu wa afya jina limehifadhiwa anasema pombe hizo ni hatari hasa kwa wanaokunywa bila kula kwani zina nguvu kubwa, ni chanzo cha wanywaji kuzidiwa na kupoteza maisha.

Kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali Teule ya Nyerere, Emiliana Donald anasema kwamba kilichosababisha kifo cha Thomas ni unywaji wa pombe kupita kiasi na madhara yake kiafya ni makubwa ikiwemo vifo.

Matukio mengine yatajwa

Miongoni mwa matukio yametajwa kuwa ni pamoja na vijana walioshindana na kuzidiwa huku wakijisaidia haja ndogo na kubwa ovyo hadi waliposaidiwa huku wadhamini wa mashindano hayo wakidai wao wameshaandaa fedha ya sanda.

Kijana mmoja maarufu aliyekuwa Dj inadaiwa kwamba alipoteza maisha katika shindano la kunywa pombe zile za kuwekwa kwenye vifuko vya plastiki, huku mpiga debe mmoja Mukunyi Mororo akiponea chupuchupu na amelazwa hospitali Teule ya Nyerere.

Kamanda aonya

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki anakiri kuwa watu wanne wanaodaiwa kuwa wadhamini wa mashindano hayo wanashikiliwa na wengine wanasakwa baada ya kutajwa kuhusika na uchunguzi ukikamilika na kubainika kuhusika watafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

DC aapa

Katika hatua nyingine, mkuu wa wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu ameapa kuwashughulikia wote wanaojihusisha na vitendo vya kucheza kama hivo