HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 12 Aprili 2018

Azam kuishusha Yanga?

Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC imefunguka na kudai watatumia mchezo wao dhidi ya Ruvu Shooting leo kama sehemu ya kuwapa furaha mashabiki wao kwa kuibuka na ushindi wa alama tatu nasio vinginevyo.

Hayo yamebainishwa na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Idd Nassor Cheche ikiwa yamebakia masaa kadhaa kushuka dimbani kuwavaa wenyeji wao hao katika dimba la Mabatini Mkoani Pwani majira ya saa 10:00 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

"Mashabiki waje kwa wingi kutupa sapoti, sisi hatutawaangusha tutawapa kile wanachotarajia kwa kuibuka na ushindi dhidi ya Ruvu Shooting, tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejipanga kukabiliana na hilo ili kupata pointi tatu", amesema Idd Nassor.

Aidha, Azam FC itaendelea kuwakosa mabeki wake, Yakubu Mohammed, Daniel Amoah, David Mwantika na washambuliaji Shaaban Idd, ambao bado ni wagonjwa huku mshambuliaji Wazir Junior, akiwa tayari ameanza mazoezi na wenzake  baada ya kumaliza siku tano za mapumziko za kumalizia matibabu ya kifundo chake cha mguu.

Timu ya Azam FC endapo itafanikiwa kutoka na ushindi katika dimba la Mabatini itakuwa imejiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kwa kuweza kuwashusha mabingwa watetezi wa ligi, Yanga nafasi moja huku wakiwa wanatofautiana kwa idadi ya magoli ya kufungwa na kushinda.