Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Nshoma Shija anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 mkazi wa Kitongoji cha Mabu,kijiji cha Shabuluba kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga (Vijijini) mkoa wa Shinyanga ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.
Malunde1 blog imeambiwa kuwa mwanamke huyo ameuawa akiwa nyumbani kwake wakati anapika viazi nje ya nyumba yake majira ya saa moja usiku huu Jumamosi Aprili 21,2018.
Taarifa zaidi tutawaletea