DIAMOND PLATINUMZ AANIKA SIRI NZITO,NI BAADA YA MASWALI KIBAO YA WABONGO
Msanii mkubwa Tanzania wa Muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, amefunguka na kusema kuwa watu wamekuwa wakimsema kuwa anavaa msalaba ambao hauendani na imani yake lakini ukweli unabaki kuwa siri ya msalaba huo anaijua yeye na kwamba kwake yeye ule sio msalaba bali ni alama ya kumjumlisha ambayo kwake ina maana sana.
Diamond amesema hayo kwa sababu kuna kipindi aliwahi kuongelewa hadi na viongozi wa dini kuwa amekuwa haeleweki kwa sababu anavaa misalaba ambayo ni kunyume na imani ya dini yake ya kiislamu. “Cheni ninayovaa na watu kunidisi kwamba ni msalaba kiukweli huwa ninashangaa sana kwa maana watu huzungumza kile ambacho hawakifahamu.
Kwangu huo si msalaba, bali ni alama ya jumlisha ambayo ninaona haina tatizo lolote, kwani alama hiyo inamaana kubwa kwangu ambayo itabaki kuwa siri yangu!”Aliongea Dimaond akichonga na kipindi cha Mikito Nusu Nusu cha GPL