HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 22 Aprili 2018

DIAMOND PLATNUMZ ASABABISHA KIZAA ZAA, SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MASOGANGE.

DIAMOND PLATNUMZ ASABABISHA KIZAA ZAA, SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU MASOGANGe

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Fleva na kiongozi wa kundi la Wasafi ‘WCB’, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, amesababisha kizaa zaa kwenye viwanja vya Leaders, katika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu Agnes Gerald Waya, maarufu kwa jina la Agnes Masogange.

Diamond amesababisha kizaa zaa hicho mara baada ya mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Steven Nyerere, kumkaribisha kwaajili ya kutoa salamu zake za pole kwa wafiwa na watu wote walikuwa kwenye viwanja hivyo.

Mara baada ya kusikia Diamond anakuja kuzungumza, waandishi wa habari waliokuwa kwenye viwanja hivyo, walianza kuvuruga utaratibu na kutoka sehemu walizokuwa wamepangiwa kueleke sehemu aliyokuwa Diamond.

Diamond akiwa amekaa pamoja na waombolezaji wengine

Mara baada ya kutokea tafrani hiyo, ndipo MC Pilipili, aliyekuwa mshereheshaji wa tukio la kuagwa kwa mwili wa Masogange, kwa kushirikiana na Steven Nyerere, walipowaomba waandishi wa habari hayo kurudi sehemu zao za awali, ili shughuli zingine ziweze kuendelea ikiwemo msanii Diamond kutoa salamu zake za pole.

Baada ya maelezo hayo, waandishi wa habari waliweza kurudi kwenye sehemu zao, na hivyo kutoa nafasi kwa Diamond kuweza kuzungumza, ambapo amesema amsesikitishwa sana na kifo cha Masogange, huku akiwasii wasanii wenzake kumkumbuka Mungu katika enzi za uhai wao ili waweze kujitengenezea makao mema mbinguni, endapo safari yao itafika.