HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 14 Aprili 2018

Kisa Azam,kocha wa Barcelona ahusishwa Ruvu shooting




Kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amtaja Kocha wa FC. Barcelona, Ernesto Valverde.

Msemaji alitamba kwa kusema kuwa Kocha huyo alipaswa kuwepo ili awashuhudie vijana wake namna walivyoupiga dhidi ya Azam na kupelekea kupata matokeo hayo.

Bwire ameeleza kuwa kikosi chake kilicheza mchezo wa kuvutia na kuwafanya Azam washindwe kuhimili mikiki yao Uwanjani.

Mabao ya Ruvu yamefungwa na Khamis Mcha katika dakika ya 29 kipindi cha pili huku bao la pili likifungwa na Fully Maganga kwenye dakika ya 80 kipindi cha pili.

Ushindi huo wa jana uliwafanya Ruvu Shooting wapande mpaka nafasi ya saba katika msimamo kwa kufikisha alama 29 huku wakiwa wamecheza michezo 24.

Azam iilikubali kipigo hicho na kuendelea kusalia nafasi ya tatu msimamoni mwa ligi ikiwa na pointi zake 45.