KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa ameeleza namna ambavyo wamemkamata na kumhoji msanii maarufu Nassib Abdul a.k.a Diamond na kisha kumuachia kwa dhamana.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam na Michuzi blog,Kamanda Mambosasa amesema alimakata Diamond jana kati ya saa 11 na saa 12 jioni na kisha walimhoji kutokana na kusambaza picha za utupu katika mtandao.
"Polisi tumemshikilia Diamond na kisha tukamhoji kwa kusambaza picha za utupu mtandaoni,"amesema Mambosasa na kuongeza kuwa hilo ni kosa la kimtandao hivyo sheria itachukua mkondo wake.
Alipoulizwa kama Diamond bado anashikiliwa Polisi au laa, Mambosasa amejibu baada ya kumhoji walimuachia kwa dhamana wakati upelelezi ukiendelea."Upelelezi ukikamilika tutaendelea na hatua nyingine za kisheria,"amesisitiza.