Manchester United imekubali kichapo cha bao 1-0 ikiwa nyumbani Old Trafford kutoka kwa West Brom.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na Rodriguez katika dakika ya 73 ya kipindi cha pili.
Matokeo yameifanya United iendelee kusalia kwenye nafasi ya pili ikiwa na alama 71 huku ikicheza michezo ya ligi 33 mpaka sasa.