HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 6 Aprili 2018

Mtibwa sugar yatuma salami kwaSimba

Mtibwa sugar yatuma salami kwaSimba


Mtibwa Sugar imeifanyia mauaji Singida United kwenye dimba lake la Namfua kwa kuilaza mabao 3-0 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 23.

Singida United imekumbana na kipigo hicho siku tatu tu tangu iondoshe Yanga kwenye michuano ya kombe la FA kwa mikwaju ya penati 4-3 kwenye uwanja huo huo baada ya sare ya bao 1-1.

Lakini leo vijana hao wanaonolewa na kocha Hans van Pluijm walionekana kuelemewa kila idara ya Mtibwa Sugar iliyofunga mabao yake kupitia kwa Sabato, Kihimbwa na Dilunga aliyefunga kupitia mkwaju wa penati.

Nayo Mbao FC imelazimishwa suluhu ya 0-0 na Lipuli FC kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Mwadui FC dhidi ya Majimaji kupigwa.

Mtibwa Sugar itaikabili Simba siku ya Jumatatu April 09 kwenye mchezo wa kiporo utakaopigwa kwenye uwanja wa Jamhuri.