Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amefunguka na kusemakitendo cha Kambi rasmi ya upinzani bungeni kugoma kuleta hotuba bungeni kwa kigezo cha kutokuwa na watumishi wa kuwaandikia hotuba hizo siyo sawa na kudai hata watumishi wa kambi ya CCM wamefukuzwa pia.

Ndugai amesema hayo leo bungeni April 17, 2018 na kusema wameona watumishi hao ambao walikuwepo kwa mikataba ya miaka miwili miwili wasiwepo na kazi za kundika hotuba hizi zifanywe na wabunge wenyewe.
"Tuna kambi mbili kambi ya Chama tawala na Kambi rasmi ya Upinzani, chama tawala walikuwa na watumishi watano wanaowaleta wao wenyewe kwenye ofisi ya CCM ya kwao hapa bungeni na tumekuwa tukiwapa mikataba ya muda mfupi walipata ya miaka miwili na nusu na sasa walitakiwa kama utaratibu huo unaendela wapate miaka miwili na nusu tena na kambi ya upinzani ni hivyo hivyo pia wao walikuwa na watumishi wanne ambao nao ni wa mkataba wa muda sasa mkataba ule uliisha na uliishia Disemba 2017. Amesema Ndugai
Akaendelea zaidi Ndugai, " kwa sasa tunadhani ni vizuri watumishi wa namna hiyo wasiwepo kwa hiyo hata watumishi wa CCM wameshafungishwa vilago hawapo na watumishi wa upinzani hawapo kwa hiyo kuendelea kugoma kuleta hotuba kwa kisingizio kwamba hakuna wa kutuandikia maoni yangu ni kwamba tunajishusha kidogo wabunge naamini kabisa tunaweza kuandika hotuba zetu kwa hiyo tuandike tu hotuba zetu" alisema Ndugai
Aidha Ndugai aliendelea kusema kuwa kama kutakuwa na hoja ya msingi juu ya jambo hilo basi wanaweza kukaaa na kuzungumza katika vikao vingine ili wasijadili hilo bungeni kwani anaamini watu watadaka hilo kuwa kuna wabunge ambao hawawezi hata kuandika hotuba zao wenyewe