Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefunguka na kumshukuru msanii Alikiba kwa kumtembelea nyumbani kwake leo na kusema kuwa amempa taarifa kuwa ataoa hivi karibuni.
Kikwete amesema hayo leo April 14, 2018 kupitia mtandao wake wa twitter na kusema kuwa msanii huyo ambaye sasa bado anafanya vyema na wimbo wake wa 'Seduce me' amemwambia anatarajia kuoa siku za karibuni.
"Namshukuru Alikiba kuja kunitembelea na kunitaarifu kuwa anatarajia kuoa hivi karibuni. Nimempatia nasaha zangu na kumtakia kila la kheri kwa jambo hilo jema aliloamua kufanya" alisema Kikwete