HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

Salamba azishushua Simba,Yanga usajili


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Lipuli FC, Adam Salamba.

 Kauli hiyo ni kama imeziumbua klabu kongwe nchini, Simba na Yanga ambazo zimetajwa kuifukuzia sahini ya nyota huyo.

Salamba amekuwa maarufu baada ya kuifungia timu yake bao katika mechi dhidi ya Simba wiki iliyopita na vile vile alibuka Mchezaji Bora wa mwezi uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara na 

Akizungumza na gazeti hili, Salamba, alisema anahitaji kuona anaendelea kupata nafasi zaidi ya kucheza na si kukimbilia kusajili klabu ambayo itamfanya akae benchi kwa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo alisema pia atahakikisha anaichezea timu itakayompa maslahi mazuri kwa sababu anahitaji kujiendeleza na kumlea mama yake.

"Ni kweli nimeshaanza kufuatwa na timu kubwa, lakini sitakurupuka kuingia mkataba bila ya kuhakikisha kuwa na namba ya kucheza, sitaki kupotea, nahitaji kuona ninapata nafasi ya kucheza na kuonekana na makocha zaidi wa ndani na nje ya Tanzania," alisema Salamba.

Aliongeza kuwa kwa sasa anajipanga kuendelea kuitumikia Lipuli kwa nguvu na hatimaye kumaliza katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo inatarajiwa kumalizika ifikapo Mei 26 mwaka huu.