HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 30 Aprili 2018

Sikujua hata Ulaya kuna wajinga na wafuata mkumbo wa kisiasa!


Na. Jamiiforums.com

Kilichotokea juzi kimenifumbua macho na kunipa elimu zaidi kuhusu watanzania wanaoishi ughaibuni.

Ninakumbuka tulichekwa sana baada ya aliyekuwa anajiita Mchungaji Kibweterere kuwafungia waumini wake ndani ya kanisa na kulichoma moto kwa madai kuwa umefika wakati wao wa kwenda mbinguni!

Nilikuwa ninafahamu kuwa vigezo vya watanzania wengi kwenda Ulaya ni elimu. Kwa maana nyingine wameelimika!

Nilikuwa ninadhani wajinga na wafuata mkumbo wanapatika katika ukanda huu pekee lakini vipererushi walivyokuwa wamebeba wafuasi wa Mange Kimambi huko Ulaya kilinifundisha mengi.

Fikiria mtu amebeba bango lililoandikwa "Rais Magufuli amemuua Mwangosi". Rais Magufuli na kifo cha Mwangosi wapi na wapi?

Ninaweza kumsamehe na kumpa ''benefit of doubt'' kuhusu Rais Magufuli kumuua Ben Saanane kwa sababu sifahamu Ben saanane alipo. Inawezekana yeye ''anafahamu vizuri''!

Inafahamika kuwa Mwangosi aliuwawa wakati wa Utawala wa Rais Kikwete lakini kwa vile mbeba bango ni mjinga au hajui hata historia ya matukio ya kisiasa nchini alijikuta akifuata mkumbo au alibeba bango bila hata kujua kilichoandikwa kwenye bango.

Mtu kama huyu aliyebeba bango unajiuliza kama hata alijua kwa nini yuko kwenye maandamano.

Kila siku tunasikia watu wanaoishi ulaya wakituambia "make an intelligent informed decision before taking action''.

Kuna wengine hata kuimba wimbo wa taifa hawajui lakini walikuwa wanadai ni Watanzania wazalendo wanaolipigania taifa.

Kumbe hata Ulaya kuna wajinga na wafuata mkumbo!