HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 26 Aprili 2018

Vigogo wa yanga watua Morogoro

Vigogo wa klabu ya Yanga wameweka kambi ya siku moja mjini Morogoro kwa lengo la kuweka sawa mikakati ya timu yao kufanya vizuri katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Simba.

Mabosi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya usajili, Hussein Nyika pamoja na Mjumbe wake, Salum Mkemi, walifika mpaka uwanja wa Highland kuangalia mazoezi ya timu yao.

Nyika alisema kuwepo wao Morogoro kumewaongezea motisha wachezaji wake baada ya kuzungumza mawili matatu kabla ya mchezo.

"Hatukuja huku tangu walivuoweka kambi, uwepo wetu huu ni mzuri na tumewapa motisha kuelekea mchezo huu lakimi hatuwezi kuweka wazi kwasasa," alisema.

Wakati huohuo; 

Wachezaji Ibrahim Ajib, Amisi Tambwe, Andrew Vincent na Thabani Kamusoko wamejiunga na wenzao mkoani Morogoro kwaajili ya maandalizi dhidi ya watani wao wa jadi Simba utakaopigwa Aprili 29.

Katika mazoezi hayo yaliyokuwa yanasimamiwa na Kocha Noel Mwandila pamoja na Shadrack Nsajigwa, walionekana kuwa wakali muda wote huku wakiwataka wachezaji hao kutekeleza yale waliyohitaji

Mwanaspoti