HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 28 Aprili 2018

VIONGOZI, WANACHAMA 800 WA UPINZANI WAHAMIA CCM


takribaini 800 wakiwemo viongozi wa vyama vya upinzani vya Chadema na CUF katika jimbo la Kondoa Mjini, wamehamia Chama cha Mapinduzi-CCM.

Hayo Wanachama yamesemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini, Edwin Sanda  wakati akitoa salamu kwenye hafla ya uzinduzi wa barabara kuu ya Dodoma kwenda Bababati mkoani Manyara.

Amesema wananchama hao wamehamia CCM kwa nyakati tofauti kutokana na kuridhishwa na kazi anayoifanya Rais John Magufuli.

“Wanachama 800 wamehamia kwetu, katika jimbo la Kondoa ilikuwa kata moja ya upinzani ambayo diwani wake alihamia CCM na kupewa kadi, safu ya uongozi mzima wa Chadema imehamia CCM. Tunakwenda kubomoa moja kwa moja dhana ya upinzani Kondoa kutokana na kazi kubwa unayoifanya,” amesema.