WANAFUNZI WASIO KWENYE MFUMO RASMI WAKUMBUKWA- Taasisi ya Elimu ya Watu wazima imesema kwa sasa wanafunzi wote wanaosoma Shule za Sekondari kwa mfumo usio rasmi, watakuwa na mitaala yao katika masomo ya sayansi ya fizikia na kemia tofauti na ilivyokuwa awali.
Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo wamesema hayo wakiwa wanafunga warsha ya kuandaa muhtasari wa masomo ya fizikia na kemia ambayo itasaidia wanafunzi wasio kwenye mfumo rasmi.
Vitabu vitano ndivyo vitakavyotumika katika awamu ya kwanza ambapo kwa kawaida Kidato cha Kwanza ndiyo wataanza kukaguliwa ambapo wito umetolewa kwao kuanza kutumia mtaala huo.
DOWNLOAD KATISHA BLOG APP
BONYEZA HAPA CHINI