HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 17 Aprili 2018

WAZIRI MBARAWA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA (TPC) KUKAGUA UTENDAJI


WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Profesa Makame Mbarawa (MB) leo tarehe 17 Aprili, 2018 amefanya ziara ya kushtukiza Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania.

Mhe. Profesa Mbarawa ametembelea Makao Makuu ya Shirika la Posta Tanzania kwa lengo la kukagua utendaji na uendeshaji wa shughuli mbalimbali za Posta, katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliongozana na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Posta Luteni Kanali mstaafu Dr. Haruni Kondo.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri alitaka kujionea matumizi ya mifumo ya kielektronik na namna ambavyo Shirika limejipanga kuitumia mifumo mbalimbali ili kusimamia utendaji kwa ukaribu. Mhe. Waziri Mbarawa alitembelea idara ya Fedha, Idara ya Barua na Logistiki, Idara ya Sheria, Idara ya Masoko na pia alikagua mifumo udhibiti wa gharama za mafuta na mwenendo wa magari ya Shirika yanayosafiri kati ya Dar es salaam na mikoani

Katika ziara hiyo Mh. Waziri ameitaka menejimenti ya Shirika kusimamia utendaji kazi na kuzingatia weledi na matumizi ya mifumo ya kielektroniki na kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati), akizungumza na Uongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati alipofika kwenye Ofisi za shirika hilo, kukagua utendaji katika Idara mbalimbali za shirika hilo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiangalia baadhi ya mikataba iliyoingiwa na shirika hilo
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta, Agnes Mtango. Kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akielekeza jambo katika Idara ya Kompyuta ya Shirika la Posta. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo, Dk. Haruni Kondo na kushoto ni Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe
Afisa Msimamizi wa Magari ya Shirika (Transport Officer), Mhandisi Lameck  Francis (kulia), akimweleza Waziri Profesa Mbarawa namna ya mfumo wa Udhibiti wa magari na mafuta kwenye moja ya kompyuta za idara hiyo, unavyofanyakazi.