Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Highlinds mkoani Morogoro kikijiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba.
Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema wachezaji wote waliokuwa majeruhi wako tayari kurejea kikosini baada ya kupona.
Wakati wengine wakianza mazoezi hapo jana, wachezaji Obrey Chirwa, Donald Ngoma na Papi Tshishimbi wanatarajiwa kuungana na wenzao mkoani Morogoro leo.
Aidha ujio wa kocha Mpya Mwinyi Zahera umeongeza 'mzuka' kwa kikosi cha Yanga.
Katika hatua nyingine, klabu ya Simba ililazimika kuhama uwanja wa Highlands waliokuwa wakiutumia baada ya Yanga kuwasili.
Simba walivamia uwanja huo ambao Yanga tayari walikuwa wameulipia.
Yanga imekuwa ikiweka kambi mkoani Morogoro na kutumia uwanja huo kwa mazoezi.