HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 27 Aprili 2018

YANGA: SIMBA HAWATAAMINI J’PILI


KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wengi hawataamini kitakachotokea keshokutwa Jumapili, kwani wamepanga kushangaza mashabiki wanaowabeza kuelekea mchezo huo.
Yanga, wenye pointi 48, watavaana na watani zao, Simba, Jumapili, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameweka kambi mkoani Morogoro, huku wakifanya mazoezi katika Uwanja wa Highland, mkoani humo.
Akizungumzia maandalizi yao, Nsajigwa alisema wamekuwa wakijinoa vema kuhakikisha wanaondoa udhaifu uliojitokeza kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Mbeya City, waliolazimisha sare ya bao 1-1.
“Maandalizi yanaendelea vema, mashabiki wetu wanatakiwa kuendelea kutupa sapoti ili katika mechi hiyo ya Jumapili tupate ushindi mzuri utakaotuweka katika mazingira mazuri kwenye mbio hizi za ubingwa na kuwashangaza wapinzani wetu wasiamini kitakachotokea.
Naye beki Kelvin Yondani, aliwataka wachezaji wenzake kila mmoja kuweza kupambana kwa hali na mali, kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo huo.
“Kikubwa tunataka kuendelea kuweka heshima ili tuwashangaze watu, kwa sababu kila mtu anaamini kuwa tayari Yanga imeshafungwa, hivyo kila mmoja wetu apambane kuhakikisha tunaibuka na pointi tatu,” alisema Yondani.
“Kwa upande wangu nimepanga kutimiza majukumu yangu vizuri pamoja na mabeki wenzangu kuhakikisha tunaokoa na kupunguza hatari langoni kwetu na hatutaruhusu bao,” alisema.
Kwa upande wake, Nahodha Nadir Haroub Cannavaro alisema kuwa: “Soka ni mchezo wa makosa, hivyo tulishakosea kwa Mbeya City hatutaki kurudia makosa hayo, badala yake tutapambana kwa nguvu ili tushinde”.
Mechi ya watani hao wa jadi itachezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare walipokutana mzunguko wa kwanza.

NSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO

    bonyeza hapa chini uwe wakwanza kuhabarika
INSTALL KATISHA BLOG KWENYE SIMU YAKO
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD KATISHA BLOG APP IN GOOGLE PLAY STORE ...ANDIKA KATISHA ...SEARCH