KATISHA BLOG
Licha ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Singida United leo, bado mbio za ubingwa ziko wazi. Simba inaongoza tu kwa tofauti ya alama tano.
Matokeo ya ushindi leo yangeongeza presha kwa Simba ambayo itashuka uwanja wa Taifa kesho kuikabili Mbeya City.
Iwapo Yanga itaweza kuifunga Simba zitakapokutana April 29, bado itakuwa na nafasi ya kutetea ubingwa wake.
Ikumbukwe Simba bado italazimika kuifuata Singida United mkoani Singida kwa ajili ya mchezo wa marudiano.
Mchezo huo pia hautakuwa rahisi kwa Simba kwani sidhani kama Singida United itakubali kupoteza mara mbili dhidi ya Simba.
Singida United imekuwa ikiikamia sana Yanga kutokana na ukweli kwamba kocha Hans alikuwa Yanga kabla ya kutua Singida.
Yanga isahau matokeo ya leo na ielekeze nguvu kwenye mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaitta Dicha Jumatano ijayo.
Yanga inakaribia kabisa kutinga hatua ya makundi na ikifanikiwa kufanya hivyo itajinyakulia kitita cha zaidi ya Mil 600.
Pesa ambazo ni karibu mara nane ya pesa za kutwaa ubingwa wa VPL.
Hapa kipaumbele kiwekwe kwenye kuzikamata pesa hizo ili ziweze kutatua matatizo ya hapa na pale klabuni.