HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 2 Mei 2018

Aliyewatumbua wenye elimu ya darasa la saba asimamishwa kazi

Kaimu Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli mkoani Tanga, Protas L Dibogo amesemamishwa kazi akituhumiwa kukaidi agizo la serikali la kuwarejesha kazini baadhi ya watumishi ambao waliondolewa kimakosa kwa kutokuwa na elimu ya kidato cha nne.

Uamuzi wa kusimamishwa kazi umetangazwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Peter Nyalali wakati akizungumza na watumishi waliosimamishwa kazi, huku akiwahakikishia kuwarejesha kazini kama serikali ilivyoagiza.

“Masharti yanaonyesha kwamba nyie mmeanza tarehe moja mwezi wa tano. Yeye anapotosha hapa anasema mmeanza mwezi wa sita. Ninamsimamisha kazi kuanzia tarehe ya leo na nafasi yake atakaa Bi Asha Majid,”alisema Mkurugenzi Nyalali.

Kutokana na hatua hiyo, watumishi waliokuwa wameondolewa walionyesha furaha kubwa kwa uamuzi huo wa serikali wa kuwaruisha kazini, lakini walitoa malalamiko yao kuhusu kuibiwa kwa baadhi ya nyaraka kutoka katika mikataba yao ya kazi jambo ambalo linawaweka hatarini.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Utumishi wa Wilaya ya Bumbuli, Protas Dibogo alikiri kuwa amesikia taarifa za kusimamishwa kazi na anasubiri barua ili aweze kuiandikia mamlaka husika ili apatiwe ufafanuzi.

“Ni kweli nimesimamishwa kazi siwezi nikaliongelea. Nikipata barua nitaiandikia mamlaka husika na watatoa ufafanuzi zaidi,”alisema Protas.