HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Alhamisi, 10 Mei 2018

Zamaradi Afunguka Steve Nyerere Kutafuna Michango ya Masogange


Siku moja baada ya msanii Steve Nyerere, kudaiwa kutafuna michango ya msiba wa Agnes Masogoange, aliyekuwa mweka hazina Zamaradi Mketema amesema hakuna ukweli wowote katika madai hayo.

Akizungumzana na MCL Digital leo Mei  10, amesema fedha hizo Sh2.1 milioni, anazo yeye na wanachosubiri ni kupata taarifa sahihi za mtoto wake Sania Sabri, kutoka kwa familia ili wamhifadhie benki.

“Jamani wanamuonea tu Steve wa watu, mbona hela ninazo mpaka sasa, kilichopo hapa ni mawasiliano na familia ili kutupa taarifa kamili za mtoto kwa ajili ya kutusaidia mchakato wa kumfungulia akaunti.

“Pia ieleweke uamuzi wa kufungua akaunti ya mtoto haukutolewa na Steve bali na kamati iliyokuwa ikisimamia shughuli zote za mazishi,” amesema.

Juzi akihojiwa katika moja ya kituo cha redio, ndugu wa baba wa mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Sada, alisema mpaka sasa hawajapata michango hiyo na wala hawana mawasiliano na kina Steve, jambo lilizua gumzo mitandaoni.

Hata hivyo, Steve aliyekuwa mwenyekiti wa kamati hiyo alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alisisitiza kuwa fedha hizo hatopewa mtu mkononi bali atafunguliwa mtoto akaunti ili zimfae wakati akianza kidato cha kwanza mwakani.

Masongane alifariki Aprili 20, mwaka huu, akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Mama Ngoma, na kuzikwa Aprili 23 kijijini kwa baba yake Utengule, mkoani Mbeya.