Michuano ya SportPesa Supercup mwaka huu itafanyika nchini Kenya ambapo inatarajia kuanza Juni 03 mpaka Juni 10 jijini Nairobi katika dimba la Kasarani.
Mkuregenzi wa SportPesa Tanzania Abasi Tarimba amesema bingwa wa michuano hiyo itakayohusisha timu kutoka Tanzania na Kenya atajinyakulia kitita cha dola 30,000 (Tsh Mil 68) pamoja na kupata nafasi ya kwenda nchini Uingereza kucheza na klabu ya Everton kwenye dimba Goodison Park.
Jumla ya timu nane zitashiriki mashindano ya mwaka huu ambazo ni Simba, Yanga, Singida United na JKU kutoka Tanzania sambamba na Gor Mahia, AFC Leopards, Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboys kutoka Kenya.
Mwaka jana klabu ya Gor Mahia ilitwaa taji la michuano hiyo iliyofanyika nchini Tanzania na kucheza dhidi ya Everton kwenye uwanja wa Taifa.