HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 22 Mei 2018

Breaking News: Chalinze: Mabosi watatu wa Tanzania investment centre, wafariki ajalini

Habari za usiku wadau kuna ajali mbaya iliyotokea leo usiku maeneo ya Chalinze na kugharimu maisha ya Mabosi watatu wa TANZANIA INVESTMENT CENTRE.

Mabosi hao walikuwa wanaelekea Dodoma kwenye mkutano/Kikao muhimu kilichokua kifanyike Kesho Jijini Dodoma.

Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).

Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus. Mwenyezi Mungu aziweke roho za Marehemu mahali pema peponi na awaponye majeruhi wa ajali hii mbaya.