HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 1 Mei 2018

Ishu ya Tshishimbi iko hivi

Na.mwanaspoti.co.tz

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema walilazimika kumtoa kiungo wao Mkongomani, Papy Tshishimbi, katika mechi dhidi ya Simba juzi Jumapili kwa sababu hakuwa sawa.

Nsajigwa ambaye alisaidiwa na Mzambia, Noel Mwandila, kuiongoza Yanga iliyopokea kipigo cha bao 1-0 , alimfanyia Tshishimbi mabadiliko katika kipindi cha pili jambo lililowashangaza mashabiki wa timu hiyo walioamini kiungo huyo alikuwa anacheza vizuri.

“Unajua watu wanapenda kuzungumza vitu wasivyovijua. Hakuwa kwenye kiwango chake kwa sababu ya majeruhi, alicheza mechi ile akitokea kwenye majeraha,” alisema Nsajigwa ambaye ni nahodha na beki wa pembeni wa zamani wa kikosi hicho.