
Licha ya kila mchezaji kati ya hao saba kuwa na sababu ya kutokuwepo kikosini, taarifa ziÂnasema wachezaji hao hawapo kikosini wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi ya nyuÂma.
Wachezaji hao saba ni mbali ya Amissi Tambwe na Donald NgoÂma ambao ni majeruhi wa muda mrefu katika kikosi cha timu hiyo kongwe nchini ikiwa imeanÂzishwa katika miaka ya 1930.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
Yanga imecheza na USM Alger bila ya nyota hao ambao kwa hakika wangeongeza kitu katika mchezo huo wa Kombe la ShirikÂisho.
Suala la kudai kwa wachezaji wa Yanga halikuanza ghafla, bali ni kitu cha muda mrefu amÂbacho kingeweza kutatuliwa ama kwa kuwaeleza ukweli wachezaji au kuita wadau wenÂgine ili wasaidie.
Uongozi wa Yanga ungezunÂgumza wazi kwamba hauna fedha za kuwalipa wachezaji hao kwa sasa na hata wacheÂzaji wangejua lakini ahadi isiyoÂtekelezeka imekuwa fimbo ya mgomo baridi huu wa sasa.
Wachezaji hawa nao ni binadaÂmu wanaotegemewa na familia zao ambao soka ndiyo kila kitu kwao, sasa wasipopata mshaÂhara inaweza kuwa kikwazo cha kuendesha maisha yao.
Yanga ina wanachama wengi wenye fedha zao lakini kama uongozi unakaa kimya bila ya kuwafuata na kuwaeleza ukweli kuhusu nafasi ya klabu kiuchumi kamwe hawawezi kutoa choÂchote.
Kila mahali hali ya kifedha ni mbaya, hivyo ni jukumu la Yanga kuwa wakweli ili waweze kupaÂta msaada na hili ni somo kwa timu nyingine ambazo hazipendi kueleza ukweli wa mambo kaÂtika timu zote
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇