HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 21 Mei 2018

Mnyika awataka viongozi wa Chadema kuondoa hofu

Shinyanga. Naibu Katibu Mkuu Chadema, John Mnyika amewataka viongozi wa chama hicho Mkoa wa Shinyanga kuishi bila hofu badala yake waendelee kusimamia maendeleo na haki za wananchi.

Mnyika aliyasema hayo kwenye kikao cha viongozi cha mashauriano kilichofanyika juzi mkoani hapa ambapo alisema utawala uliopo unalenga kujenga hofu kwa vyama vya upinzani.

“Kuna watu wanatishwa, wanabambikizwa kesi za hapa na pale, kushambuliwa hali ambayo inawafanya viongozi kuwa na hofu na kushindwa kukemea ufisadi,” alisema

Aliongeza: “Nawasihi viongozi wenzangu tusikubali kutiwa hofu kwani tukikubali tutawahalalisha kubaki madarakani.”

Alisema serikali ya awamu hii imeshindwa kutekeleza kero za msingi za wananchi, kwani imeweka kiasi kidogo cha fedha kwenye mahitaji ya msingi ya wananchi maskini.

Alisema kutokana na hali hiyo Rais anapaswa kutoa kauli, kwani anaposema amepambana na ufisadi huku wananchi wakiteseka na hali ngumu ya maisha anatakiwa ajitokeze aseme fedha hizo za ufisadi zilizokusanywa ziko wapi maana inaonekana zimekusanywa na kutafunwa pia.

Kadhalika Mnyika alisema kama kweli wabunge wa CCM wapo kwa ajili ya kuwatetea wananchi, wakubali katiba mpya ili Tanzania iwe na maendeleo.

“Hivyo tuendelee kulisimamia suala hili mpaka kuwepo na mabadiliko,”alisema.

Katibu wa Chadema Kanda ya Serengeti, Renatus Nzemo alisema serikali imesema imekusanya fedha nyingi lakini kwa wananchi hazionekani huku akihoji zinapokwenda.

Alisema licha ya sekta ya afya kutengewa fedha nyingi lakini bado hospitali nyingi hazina dawa za kutosha na wagonjwa wanaambiwa wakanunue madukani.

Makamu mwenyekiti kanda ya Serengeti, Gimbi Masaba ambaye pia ni Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Simiyu, aliwataka viongozi hao wazingatie maadili na mtiririko ili kuendelea kikijenga chama na kiendelee kusimamia vizuri miradi ya maendeleo na wananchi wake.