Serikali imeamua na inaagiza kwamba, watumishi wa umma 1,370 waliolegezewa masharti ya sifa za muundo kupitia barua ya Katibu Mkuu Utumishi ya Juni 30,2011 warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote walichokuwa wameondolewa kazini, waendelee na ajira zao.