HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 30 Mei 2018

Mrithi wa Ngoma huyu hapa

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten leo amevunja ukimya baada ya kubainisha kuwa tayari klabu hiyo imemleta mrithi wa Donald Ngoma aliyetimkia Azam FC.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Ten amemkaribisha mchezaji huyo mpya, taarifa zaidi kumuhusu zitatolewa baada ya taratibu za usajili kukamilika.

Kwa wale wanaodhani Yanga 'imechoka' na haina uwezo wa kifedha wa kufanya usajili wa maana huenda wakashikwa na butwaa pale vifaa vitakapoanza kuteremshwa Jangwani.

Viongozi wa Yanga wameamua kutoweka wazi mchakato wa usajili baada ya kubaini kuna timu zinasajili kwa kufuata kivuli cha Yanga.

Lakini hakuna shaka kwenye michuano ya SportPesa inayoanza nchini Kenya Juni 03, baadhi ya wachezaji wapya watakaokuwa wamekamilisha usajili watatambulishwa.