HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 6 Mei 2018

Mwashiuya, Mahadh wakutana na zali Algeria

Kitendo cha Yanga kuwakosa nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza kimegeuka neema kwa wachezaji wake Abdallah Shaibu 'Ninja', Juma Mahadh na Pato Ngonyani
Kuna uwezekano mkubwa nyota hao watatu wakaanzishwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya USM Alger utakaochezwa saa 2 usiku kwa saa za Algeria.
Katika mazoezi ya mwisho ambayo Yanga ilifanya jana, wachezaji hao watatu wote walikuwemo kwenye kikosi ambacho kinaonekana kitaanza kwenye mchezo wa leo.
Kikosi hicho kinaundwa na Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Andrew Vincent, Ninja, Said Juma 'Makapu', Emmanuel Martin, Pato Ngonyani, Pius Buswita, Yussuf Mhilu na  Juma Mahadh