.

Imeripotiwa kuwa kiungo fundi wa klabu ya Simba Sc Said Ndemla amesusia ofa ya mkataba mpya ndani ya klabu hiyo akidai kwasasa malengo yake ni kwenda kucheza ulaya.
Ikumbukwe awali Ndemla alienda kufanya majaribio nchini Sweden kunako klabu ya AFC Eskilstuna baada ya majaribio hayo Ndemla alirejea kuitumikia Simba Sc kwasababu hakukuwa na makubaliano baina ya pande zote mbili kutokana na Ndemla kuwa na mkataba na Simba Sc.
Habari ambazo sokaonline imezipata ni kwamba Ndemla amegomea kuongeza mkataba mpya badala yake ataelekea nchini Sweden katika klabu ambayo alifanya nayo majaribio.
Ikumbukwe mkataba wa Ndemla na Simba unaelekea ukingoni hivyo mwishoni mwa msimu huu huenda akaondoka kama mchezaji huru.