HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 1 Mei 2018

News Alert: - Arusha: Askofu mkuu wa Kanisa la International Evangelism Elihud Isangya Ashikiliwa Polisi kwa tuhuma za mauaji

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la International Evangelism lililopo Sakila ,wilayani Arumeru ,mkoani wa Arusha ,Elihudi Isangya (69) anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani hapa Kwa tuhuma za Mauaji ya kaka yake.

Wengine wanaoshikiliwa ni mdogo wake na Askofu aitwaye,Ndewario Isangya (59) pamoja na Afisa mwandamizi wa kanisa hilo,Obadia Nanyaro(60)wote wakazi wa Sakila wilayani humo.

Watuhumiqa hao Kwa pamoja walikamatwa juzi majira ya Saa 1.30 Usiku katika kijiji cha sakila wakihusishwa na tukio la mauaji ya marehemu Nixon Isangya(71) ambaye aliuawa nyumbani Kwake Moivaro kwa kupigwa na kitu chenye ncha Kali kichwaji januari 8 mwaka 2017

Kaimu kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani hapa Yusufu Ilembo amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa alikamatwa na baada ya kuhojiwa aliwataja watuhumiwa hao wanaodaiwa kuratibu mpango huo.

Ilembo alisema kuwa Polisi wanaendelea na uchungu wa tukio hilo na pindi utakapokamilika wahusika watafikishwa mahakamani

Akizungumzia tukio hilo mtoto wa Marehemu Nixon, aitwaye Jeny Nixon Isangya ameeleza kuwa baba yake aliuawa nyumbani kwake wakati huo alikuwa akiishi na Kijana mmoja aliyemtaja Kwa jina la Simon Kaaya ,.

Hata hivyo baada ya tukio hilo Kijana huyo alitoweka nyumbani hapo hadi alipokamatwa juzi siku nyumbani kwake baada ya wananchi kuizingira nyumba yake na kumfikisha kituo cha Polisi

"Huyu Kijana alienda kumwomba Marehemu baba yangu aishi naye akidai anamwonea huruma kumwona akiishi peke yake " Amesema

Ameongeza kuwa Kijana huyo aliweza kuishi na Marehemu kuanzia januari mosi mwaka Jana kabla ya kuuawa januari 8 na kukutwa mwili wake umelazwa kitandani na kufunikwa shuka huku akiwa na jereha kichwani

Hata hivyo amedai kuwa katika uhai wake marehemu baba yake alikuwa na mgogoro wa muda mrefu na Askofu Isangya kiasi cha kutosemeshana

"Ugomvi wa baba yangu na baba Askofu Isangya ni wa muda mrefu walikuwa hawaongei hadi Marehemu alipokutwa Ameuawa kikatili chumbani kwake" Amesema

Katika hatua nyingine jana majira ya saa sita usiku Askofu alifanikiwa kuachiwa huru Kwa dhamana huku watuhumiwa wenzake wakibaki mahabusu

Hata hivyo Askofu huyo amekamatwa tena mapema Leo na kurejeshwa mahabusu katika kituo kikuu cha Polisi jijini hapa wakati akisubiri taratibu za kiupelelezi

Pichani ya kwanza Askofu Isangya 
Picha ya pili marehemu Nixon kabla ya kifo chake