HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumanne, 1 Mei 2018

News Alert: - Baadhi ya waumini wa KKKT wataka Askofu Malasusa aombe radhi na Kustaafu.

Na.
jamiiforums.com

Baadhi ya waumini wa kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania(KKKT) katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani wametoa wito mzito kwa Askofu Alex Malasusa kuliomba radhi kanisa la Lutherani hapa Tanzania kwa kitendo chake cha kudaiwa kusaliti tamko kuu la Kanisa la Lutherani lililotolewa kipindi cha Pasaka mwaka huu.

Askofu Malalusa japokuwa aliweka saini kuunga mkono kuandaliwa kwa tamko hilo lakini mwisho wa siku akazuia kwa nguvu tamko hilo kusomwa katika kanisa lolote la KKKT katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo yeye ndio Askofu wake kwa sasa.

Dayoysisi ya Mashariki na Pwani katika kanisa la lutherani hapa Tanzania inajumuisha mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani na eneo lote la Zanzibar.

Waumini hao pia wamemtaka Askofu Alex Malasusa kuomba kustaafu haraka nafasi ya Uaskofu ili kulinda heshima ya kanisa na heshima yake aliyojijengea siku za nyuma katika utumishi wake kama Askofu wa Dayosisi hiyo kwa zaidi ya miaka 15 mfululizo.

Mbali ya kuwa Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Askofu Malalusa ameshawahi kuwa Askofu mkuu wa Kanisa la Lutherani hapa Tanzania kwa vipindi viwili mfululizo kabla ya kustaafu baada ya muda wake kwisha takribani miaka miwili iliyopita.

Wito huo wa hao waumini umekuja baada ya habari kuhusu kutengwa rasmi kwa Askofu Alex Malalusa kutoka kwa Baraza la maaskofu wa Lutherani hapa Tanzania kuanza kuripotiwa toka siku ya jana na vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ndani na nje ya nchi. Katika historia ya KKKT haijulikani kama tukio kama hili lilishawahi kutokea lini tena.

Waumini hao wamefananisha kitendo hicho cha kutengwa kwa Askofu Malalusa ni sawa sawa na kunguru aliyekatwa mbawa zake hivyo hatawezi kuruka tena lakini wakati huo huo amebakiwa na mdomo na miguu huku akiwa amewekwa ndani ya uzio unaomziua kutoka kutembea popote au kelele zake kusikika nje ya uzio huo

Baadhi ya waumini wa siku nyingi wa kanisa la Lutherani katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani wanasema kwa uzoefu wao wa mambo mazito yaliyowahi kuibuka katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani. Wanasema historia inaonyesha kuwa Askofu katika Dayosisi hiyo akishaguswa na tuhuma nzito ambazo ziko wazi sana na zenye mwelekeo wa kuliumiza kanisa basi ni Lazima atang'olewa kwa aibu kubwa.

Wengi wao wanakumbushia tukio la kung'olewa kwa aibu kwa Askofu Jerry Ngwamba katika Dayosisi hiyo hiyo ya Mashariki na Pwani mwanzoni mwa miaka ya 2000 baada ya kutuhumiwa kuligeuza kanisa la Lutherani kama mali yake binafsi, Kukiuka maadili na kuwagawa waumini kwa sababu mbali.

Jerry Ngwamba alivuliwa Uaskofu na Uchungaji wake kwa aibu kubwa na kukimbilia kusikojulikana mpaka sasa, japokuwa wengi wanaamini alikimbilia Marekani ambako alikuwa akiishi kabla na alikuwa na uraia wa nchi hiyo pia. Serikali ya Tanzania alitangaza kumtafuta ili kuja kumfungulia mashtaka mbali mbali. Hakuweza kukamatwa na hatma yake haijulikani mpaka sasa.

Tukio la kuvuliwa Uaskofu na Uchungaji Jerry Ngwamba lilienda sambamba na kuwavua uchungaji 'vibaraka' wake, na baadhi yao walifukuzwa kabisa katika uumini na kutengwa na kanisa. Kitu kama hichi kinadhaniwa huenda kikajirudia tena katika sakata hili la Askofu Malalusa.

Msisitizo wa waumini hao uko kuelezea kuwa, suala la Askofu Malasusa kung'olewa liko wazi sana kwa sasa kwa kuwa 'watesi' wake wote (Baraza la Maaskofu la KKKT na Baadhi ya waumini wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani wasiomhitaji tena) wamepata 'Fimbo ya chuma' ya kumcharaza.

Na ili kuepuka aibu kubwa dhidi yake, kuibuliwa tuhuma nyingine mpya dhidi yake, kupoteza muda na kuepusha kupoteza haki zake zingine za Kiimani(Uchungaji wake na Uumini wake), kiuchumi na kiheshima ni busara tu kwa Askofu Malasusa kufanya mambo haya kwa haraka.

-Kuandika barua ya kuomba radhi kwenda Baraza la Maaskofu wa Lutherani Tanzania.

-Kuelekeza ule Waraka wa KKKT wa kipindi cha pasaka usomwe sasa katika makanisa yote ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani(Hata kama muda wa kusomwa waraka ule unaonekana umepita, uzito wa maneno yake bado unaufanya waraka ule uendelee kuishi!).

-Kutangaza mchakato wa kustaafu kwake kwenye cheo cha uaskofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani kabla ya kwisha kwa mwaka huu.

Sababu za waumini wao kumuomba Askofu Alex Malalusa kutaka kuchukua hatua hizo zimesimamia kwenye msingi wa mambo matano.

1/Kutengwa kwa Askofu Malasusa na Baraza la Maaskofu katika KKKT kwa maana pana ni kutengwa kwa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambayo Askofu Malasusa anaitumikia sasa. Na kitu hicho waumini hawako tayari kukiona.

2/Maendeleo ya Dayosisi yoyote katika KKKT yanategemea pia uhusiano na Dayosisi zingine hapa Tanzania na nje ya Tanzania. (Katika hali hii waumini wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani hawako tayari kuingia gharama ya 'kumfuga' askofu Malalusa.)

3/Kitendo cha Askofu Malasusa kufanya huo 'Usaliti' wake dhidi ya waraka rasmi wa Kanisa wa Pasaka haukutokana na Askofu Malasusa kutumwa na waumini wake kwenda kuufanya, Askofu Malasusa alifanya hivyo kwa matakwa yake binafsi.(Wapo wanaoamini kuwa alikubali kutumika kisiasa, hasa hasa baada ya Paul Makonda kutamka hadharani kuwa waraka ule ameudhibiti, na haukusomwa popote Dar).
Hivyo waumini hao hawatakuwa tayari kuvuna kitu wasichokipanda. Askofu Malasusa abebe msalaba wake yeye mwenyewe.

4/Askofu Malasusa alishapoteza uungwaji mkono kutoka kwa wachungaji wake wengi na waumini wengi wa kanisa la Lutherani katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani siku kadhaa kabla kutokana na mlolongo wa tuhuma nzito zinazomuandama mara kwa mara (Katika vita hii huenda Askofu Malasusa akajikuta amesimama mwenyewe).

5/Askofu Malasusa ameshatumikia nafasi zote za juu za uongozi wa kanisa la Lutherani hapa Tanzania, tena kwa muda mrefu, hivyo busara ni kukaa pembeni kwa Amani na Heshima. Na muda huu ndio muafaka zaidi. Hata poteza chochote zaidi ya kulinda kile chema alichokipanda.

Wadadisi wa mambo wanasema huenda ni muda muafaka kwa Askofu Malalusa kwa sasa kusoma pia alama za nyakati kuwa hatakiwi tena kwenye uongozi wowote wa juu wa kanisa la Lutherani Tanzania. Na walichokifanya baraza la maaskofu ni kama kumtega tu ili kurasimisha mchakato wa kumuondoa kwa aibu lakini hapo hapo kikatiba kulinda umoja wa KKKT.

(Kwa sasa ni kama Askofu Malasusa mwenyewe amepewa nafasi ya kuamua hatma yake yeye mwenyewe, kinachofuata ni waumini katika Dayosisi ya Mashariki na Pwani kuamua hatma yake na mwisho kabisa kama bado hatakuwa ameng'oka basi Baraza la maaskofu litamng'oa kwa kutumia nguvu kubwa zaidi.)

Kwa siku kadhaa kwa sasa kumekuwa na tuhuma nyingi na nzito dhidi ya Askofu Malasusa kutoka kwa waumini wa KKKT katika Dayosisi na Pwani, tena tuhuma hizo zikisemwa wazi wazi na baadhi ya wachungaji waandamizi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani huku wakiziunga mkono.

Baadhi ya tuhuma hizo ni...
1/Tuhuma za kuwa na mahusiano ya Kingono na mchungaji mmoja wa kike wa kanisa hilo kiasi cha kuharibu ndoa ya mume wa mchungaji huyo.

2/Kitendo cha kubadilisha katiba ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani kuondoa ukomo wa muda wa kuwa askofu ili yeye kuendelea kuwa Askofu milele.

3/Kitendo cha kufanya mchakato wa kubadilisha Katiba ya Dayosisi ya Mashariki na Pwani ili isiingiliwe mambo yake ya ndani na Baraza la Maaskofu wa Lutherani Tanzania(Wakosoasi wake wanasema huko ni sawa sawa na kuitenga Dayosisi ya Mashariki na Pwani kutoka KKKT, na msimamo wake huo unapingwa pia na Maaskofu wengine wa KKKT kwa kigezo kuwa huko ndio mwanzo wa kuisambaratisha KKKT).

4/Kitendo cha kudaiwa kutoa tafsiri 'Potofu' ya kitheologia ya kuunga mkono matumizi ya Pombe kwa mkristo mlutheri(Kwa kanisa la lutherani, pombe ni haramu)