HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumapili, 13 Mei 2018

News Alert: Ripoti: Syria ilirusha makombora 56 Israel 47 yaliishambulia Israel.Netanyahu atangaza hali ya hatari

Jeshi la Syria limetoa jibu kali kwa chokochoko za utawala wa Israel kwa kushambulia kwa makombora maeneo ya utawala huo yaliyo katika miinuko ya Golan nchini Syria.
Vyombo vya habari ndani ya Israel vimeripoti kwamba, jumla ya makombora 56 yamerushwa usiku wa leo na jeshi la Syria.Makombora 9 tu yalifanikiwa kutunguliwa na Israel huku 47 yakifanikiwa kuyalenga maeneo ya kijeshi ya Israel na mengine muhimu katika miinuko hiyo ya Golan. Kufuatia radiamali hiyo kali ya jeshi la Syria, utawala huo wa Israel umelazimika kutangaza hali ya hatari huku ukiwataka walowezi wa Kiyahudi kuelekea maeneo yenye amani, huku ukifunga shule zote eneo hilo. Mbali na hayo vyombo vya Israel vimekiri kwamba, ngao ya makombora ya utawala huo, (Iron dome) imeshindwa kuzuia makombora ya jeshi la Syria suala ambalo limewalazimu makamanda wa jeshi la Israel kuitisha kikao cha dharura kujadili suala hilo.
Hii ni katika hali ambayo miripuko kadhaa ilisikika usiku wa kuamkia leo katika maeneo tofauti ya Damascus, mji mkuu wa Syria baada ya utawala Israel kutekeleza mashambulizi kadhaa mjini hapo. Sambamba na miripuko hiyo kikosi cha anga cha jeshi la Syria kimeshuhudiwa kikijibu mashambulizi hayo. Televisheni ya al-Mayadin ya nchini Lebanon imeripoti kwamba jeshi la Syria lilifuatilia makombora ya utawala wa Israel na kuyasambaratisha angani. Kwa mujibu wa habari hiyo, jeshi la Syria limefanikiwa kuangamiza asilimia 80 ya makombora yaliyokuwa yameelekezwa ardhi ya nchi hiyo. Taarifa iliyotolewa na jeshi la Syria imefafanua kuwa ndege kadhaa za kivita za Israel ziliyalenga maeneo kadhaa, ambapo akthari yazo zilitunguliwa angani. Aidha ripoti hiyo imesema kuwa, moja ya makombora hayo limeharibu jengo la kibiashara mjini Damascus.
Awali Israel ilishambulia kwa makombora mji wa Quneitra na maeneo ya Madinat al-Baath na Hader mjini hapo. Habari za hivi punde zinasema kuwa, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Utawala huo wa israel amelazimika kukatiza ziara yake mjini Moscow, Russia kufuatia jeshi la Syria kutoa pigo kali dhidi ya Israel. Habari kutoka Israel zimeripoti kwamba mashambulizi ya jeshi la Syria yameutia kiwewe utawala huo wa israel kiasi cha kuanza kulaumiana viongozi wake. Hii ni katika hali ambayo vyombo mbalimbali vya Israel vimetangaza kwamba mashirika ya kijasusi ya utawala huo, yalishindwa kufahamu iwapo jeshi la Syria lingeshambulia maeneo ya Golan na kuisababishia hasara kubwa Israel.
Nalo Shirika la upelelezi la Marekani FBI limefichua kuwa, Israel haitaki kuendeleza vita na Syria katika kipindi hiki. Kufuatia hali hiyo harakati mbalimbali za Palestina zimetoa taarifa ya kulipongeza jeshi la Syria kwa kutoa piko kali dhidi ya Israel na kuahidi kuwa upande wa jeshi hilo la Kiarabu katika kukabiliana na utawala huo wa Israel. Utawala wa nchi ya Israel umekuwa ukifanya mashambulizi ya kila mara dhidi ya taifa huru la Syria kwa lengo la kuidhoofisha serikali halali ya Damascus na kuwasaidia magaidi wa ambao wamekuwa wakishindwa kila uchao na jeshi la Syria kwa kushirikiana na wananchi
Pichani chini ni moja ya aina ya makombora syria iliyotumia kushambulia Israel
Picha ya pili mjini Damascus ambapo moja ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria ukitungua baadhi ya makombora ya Israel

Source: Parstoday