HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumamosi, 5 Mei 2018

Ngoma njia panda, Yondani, Ajib shwari



Dar es Salaam, Algers. Wakati Yanga ikiwa Algeria kuikabili USM Alger kesho, siku za mshambuliaji wa timu hiyo, Donald Ngoma zimeanza kuhesabika ndani ya klabu hiyo.

Ngoma ni miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliobaki Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali wakiwemo beki Kelvin Yondani ‘Vidic’, Ibrahim Ajib, Papy Tshishimbi na Mzambia, Obrey Chirwa.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa alimesema jana kuwa, wachezaji hao hawajasafiri si kwa kukusudia, lakini kwa sababu ya matatizo waliyonayohayo.

Mkwasa alisema, Yondani na Tshishimbi wao walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, Obrey ana malaria wakati Ajib anamwangalia mke wake anayetarajiwa kujifungua hivi karibuni.

“Kama nilivyosema, Yondani, Tshishimbi na Chirwa wao ni wagonjwa na Ajib amebaki kwa sababu mkewe anakaribia kujifungua,”alisema Mkwasa.

Wakati hali ikiwa hivyo kwa nyota hao ni tofauti kwa Ngoma amekuwa nje kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na majeruhi ya goti la kushoto jambo linalofanya uongozi wa Yanga kuweka wazi kuwa imeanza taratibu za kuachana naye.

Katibu Mkuu wa Yanga, Mkwasa alipoulizwa kuhusu Ngoma alisema hajui kiundani anasumbuliwa na nini, lakini Yanga inafanya taratibu ili waachane naye.

“Sijui kiundani Ngoma anaumwa nini, lakini mara wanasema goti mara maumivu ya misuli kwa kweli sijui lakini kuna taratibu tunafanya ili kuona tutaachana naye vipi,” alisema Mkwasa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga alipoulizwa kuhusu mpango huo wa kuachana na Ngoma alihoji mwandishi kapata wapi taarifa na alipojibiwa alidai hajui lolote.

“Sina taarifa hiyo, labda katibu (Mkwasa) anafahamu hivyo mtafute umuulize,” alisema Nyika ambaye alisisitiza wanasubiri kwanza ripoti ya kocha baada ya Ligi kuisha.

Mkataba wa Ngoma utamalizika mwishoni mwa msimu ujao baada ya kuongezewa mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu.

Daktari wa Yanga, Edward Bavu alipoulizwa kuhusu maendeleo ya Ngoma alidai anaendelea vizuri ingawa aligoma kueleza lini ataanza mazoezi.

“Masuala mengine juu ya mchezaji muulizeni Ten (Dismas ambaye ni afisa habari wa Yanga) lakini kwa kifupi ni hivyo kwamba Ngoma anaendelea vizuri,” alisema Dk Bavu.

Dokta Mwanandi Mwankema ametaja sababu tatu zinazohusiana na ugonjwa wa Ngoma kuwa ni umri, mchezaji kutopumzika na aina ya viwanja wanavyotumia.

“Ugonjwa wa goti kwa wachezaji ni mpana kidogo na sababu zake ziko nyingi, tukiachana na kugongana wenyewe kwa wenyewe lakini wachezaji kucheza muda mrefu bila kupumzika inachangia pia,” alisema Mwankemwa.

Alisema umri unaposogea pia magoti yana tabia ya kutengeneza kitu kinaitwa chokaa ambayo inasababisha matatizo ya jointi ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa Arthritis.

“Umri nao kwa wachezaji unasababisha maradhi hayo, pia viwanja vyetu mfano ule wa Karume umeharibika na kwa jinsi ulivyo ni rahisi mno wachezaji wanaoutumia kupata matatizo ya magoti,” alisema.

Dk Mwankemwa alisema ili kupunguza au kumaliza tatizo hilo mchezaji anapaswa kupumzika muda mrefu.

“Kuna yule ambaye goti linamuuma tu lakini halijateguka wala kuvunjika, huyo anapaswa kupumzika tu muda mrefu atapona, lakini kama ameteguka kupona kwake inategemea kati ya wiki nne mpaka tisa.

“Lakini kwa aliyekatika Regament atapona kati ya miezi sita mpaka tisa,” alisema

Alisema ili kuepukana na tatizo hilo, wachezaji kwanza wapumzike wawe na programu nzuri ya mazoezi na wawe na idadi ya mechi za kucheza sio kila mechi yumo.

“Mchezaji anapaswa kulala saa zisizopungua nane, watambue kuwa wanapaswa kupumzika, pia kwa uongozi viwanja wanavyotumiwa viwe bora na wenyewe kwa wenyewe wawe na ‘fair play’.

Kikosi cha Yanga kimetua salama nchini Algeria na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Algeria, Omar Yusuph Mzee.

Msafara huo umefika na moja kwa moja utakwenda katika hoteli maarufu nchini humo ya Sultane iliyo ndani ya jiji la Algiers.

Yanga itacheza mechi yake ya kwanza Kundi D Jumapili saa 4:00 usiku dhidi ya USM Alger wakati mchezo mwingine Kundi D utawakutanisha Rayons Sport dhidi Gor Mahia.