Prisons imemuongeza mkataba kipa wao namba moja Aron Kalambo na James Mwasote na kubainisha wamefanya hivyo kutokana na kutambua mchango wao.
Dar es Salaam. Uongozi wa klabu ya Tanzania Prisons umewafunga wachezaji wake Aron Kalambo na James Mwasote kwa kuwaongeza mikataba mipya.
Prisons imemuongeza mkataba kipa wao namba moja Aron Kalambo na James Mwasote na kubainisha wamefanya hivyo kutokana na kutambua mchango wao.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Katibu Mkuu wa Prisons, Oswald Morris alisema muda wa usajili bado unaendelea hivyo hawana papara kufanya usajili kwa pupa wanasubiri ripoti ya mwalimu mara baada ya ligi kuisha wanaamini watafanya usajili utakaowasaidia.
Alitumia nafasi hiyo pia kuwapongeza wachezaji wote wa timu yake kwa kuiwezesha timu hiyo kuwa katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi huku akiweka wazi kuwa msimu ujao wanaamini watafanya vizuri zaidi ya hapo.
"Unajua mpira ni mahesabu hivyo tunazichanga karata zetu upya tayari kwaajili ya msimu ujao naamini mapambano yetu yatafika mbali zaidi kama siyo kutwaa ubingwa basi kuwa katika tatu bora," alisema Morris.