Mchezo wa kwanza wa kundi D kombe la Shirikisho Barani Afrika uliozikutanisha Rayon Sports dhidi ya Gor Mahia umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Nyamirambo nchini Rwanda ulizishuhudia timu hizo zilizo kundi moja na Yanga zikigawana alama moja moja.
Yanga iko nchini Algeria ambapo Jana sa nne usiku imeambulia kichapo cha4-0 na USM Alger.