Timu ya Simba imeusogelea ubingwa wa Ligi Kuu baada ya kuifunga Ndanda FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo Jumapili.
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇
Bao la Simba lilifungwa dakika ya 44 na mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye amefikisha mabao 20.
Simba sasa wameendelea kujimarisha kileleni baada ya kunyakua alama tatu kwenye mchezo na kufikifisha pointi 65 huku wakisubiri pointi mbili tu ili kutawazwa mabingwa.
Matokeo mengine ni Stand United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azm FC mchezo ulipigwa kwenye Uwanja wa Kambarage.
Uwanja wa Majimaji, timu za Majimaji na Mtibwa Sugar zimetoshana nguvu baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.
Pia Kagera Sugar na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba mechi imemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana
PATA HABARI KWA HARAKA ZAIDI Download katisha blog App👇👇Bonyeza hapa👇👇