Wenyeji USM Algers wameanza mechi kwa kasi huku wakipeleka presha kubwa langoni kwa Yanga ambayo wachezaji wake wanaonekana kucheza kwa hofu.
Goli la Kaskazini ambalo Yanga wameanzia ndilo huwa ambalo mashabiki nguli wa USM Alger hukaa.
Mashabiki hao wamekuwa wakishangalia kwa nguvu tangu mabasi ya timu yalipokuwa yakiingia uwanjani.
Golikipa na nahodha wao Mohammed Lamine Zemmamouche ndiye mchezaji kipenzi zaidi kwenye timu hii akifuatiwa na mgungaji wa bao la kwanza Darfalou Oussama.
Wachezaji hao wamekuwa wakiimbwa kwa nguvu na mashabiki nanhata wakati vikosi vinatajwa ndio walishangiliwa kwa sauti kubwa
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->