May 26 2018 ilichezwa game ya fainali yaUEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Liverpool nchini Ukrainekatika jiji la Kyiv, game hiyo ambayo ilimalizika kwa Real Madrid kupata ushindi wa magoli 3-1 dhidi ya Liverpool na kutwaa taji la tatu mfululizo la Champions Leagueimechukua healines sana mitandaoni.
Game hiyo ilianza kwa matukio na tambo za hapa na pale za mashabiki wa soka kutaniana lakini kabla ya game kuanza picha ya Cristiano Ronaldo kumuangalia kwa kuibia Mohamed Salah wa Liverpoolilichukua headlines kiasi cha kufikia mfanyabiashara na mshabiki mkubwa sokaMohamed Dewji kuipost picha hiyo na kuandika.
“Tunaishi katika dunia ambayo imejaa watu wenye macho ya husda, macho ya fitna, macho ya unafki, na macho yaliyojaa wivu! Hakikisha unaenda na Mungu ili watu wenye macho mabaya wasiwe na nafasi ya kupenyeza ubaya katikati ya hatua zako za maisha (afya, elimu, ndoa, biashara). Ameen 🙏🏽”