Baadhi wa wakazi wa manispaa ya Mtwara Mikindani wamelalamikia kukabiliwa na hali ngumu ya kimaisha, na kudai kuwa hali hiyo inawafanya watu wengi wanaomiliki ardhi kushindwa kumudu gharama za kulipia kodi ya pango la ardhi na viwanja kwa wakati.
Wakizungumza na Clouds Tv wakazi hao wamesema vijana wengi kwa sasa wanakabiliwa na ukosefu wa ajira rasmi na zisizo rasmi ambazo zingewawezesha kupata pesa za kulipia kodi hizo.
Kwa upande wake kamishna msaidizi wa ardhi kanda ya kusini, GASPER LUANDA ameeleza kwamba bado zoezi hilo linasuasua.
Aidha kamishna LUANDA akazungumzia juu ya wamiliki wa ardhi na mashamba kupitia hati za kimila na kudai kuwa hawahusiki na kodi hizo.
Kodi ya pango la ardhi kwa wamiliki wa viwanja na mashamba ambayo ipo kwa mujibu wa sheria ya ardhi sura ya 113 kifungu cha 33, hulipwa kwa hiari kuanzia Julai mosi hadi disemba 31 ya kila mwaka.