Ukijaribu kufuatilia ziara za Rais Magufuli ndani ya nchi na msafara wake wananchi wengi sana wanajitokeza kila kwenye kijiji au miji midogo iliyopo kanda ya barabara na karibu maeneo hayo yote Rais husimama na kuwasilimia kwa muda mfupi.
Lakini kikubwa nachokiona katika ziara hizi kwanza ni ile idadi kubwa inayojitokeza na pili namna wanavyoshangilia hotuba zake na kumfurahia Rais Magufuli na tatu anavyosikiliza kero zao na zingine kuzitatua on the spot.
Hali hii unaweza kuitafsiri vipi kiutawala na haya maneno maneno ya kila siku hali ngumu kimaisha,utawala unakandamiza haki na demokrasia na kuuwa watu?