HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 7 Mei 2018

Yanga italazumika kushinda mechi zote za nyumbani

Kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya USM Alger jana hakimaanishi kuwa Yanga haina nafasi ya kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Yanga itacheza michezo mingine mitano kwenye michuano hiyo mitatu ikitarajiwa kupigwa kwenye dimba la Taifa.

Kama itaweza kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani Yanga bado ina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwani kila kundi litatoa timu mbili.

Mchezo wa kwanza wa nyumbani ni May 16 dhidi ya Rayon Sports ambayo jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Gor Mahia kwenye dimba lake la nyumbani.

Yanga inahitaji kushinda mchezo huo.

USM Alger wako vizuri

USM Alger inapewa nafasi kubwa ya kuongoza kundi D kutokana na ubora wa kikosi chake.

USM Alger mabingwa wa zamani wa ligi ya mabingwa barani Afrika, wana uzoefu mkubwa wa soka la Kimataifa kwenye ngazi ya vilabu

Ukitoa USM Alger, viwango vya Gor Mahia na Rayon Sports sio vya kutisha na Yanga inaweza kuchuana nazo kuwania nafasi ya pili.

Sio vilabu tu, hata kwa timu za Taifa, wenzetu wa Afrika ya Magharibi na Kaskazini wametuzidi mbali sana katika ubora.

Timu zetu zinahitaji uwekezaji mkubwa na maandalizi ya kutosha ili kuweza kushindana nao.