HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatatu, 14 Mei 2018

Yanga sikio la kufa

HALI bado mbaya ndani ya kikosi cha Yanga baada ya jana kukubali kipigo cha tatu mfululizo kutoka kwa Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni.

yanga.

Nyota wa zamani wa Yanga, Hassan Dilunga ndiye aliyepeleka kipigo hicho baada ya kufunga bao pekee katika dakika ya 82 akipokea pasi ya kupenyeza kutoka kwa Haruna Chanongo.

Kipigo hicho cha jana kinaifanya Yanga kuendelea kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 48 nyuma ya Azam FC yenye pointi 52 inayokamata nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Simba.

Mchezo wa jana licha ya Yanga kucheza soka la kasi wakitumia mtindo wa kufanya mashambulizi ya kushtukiza, ilibanwa vilivyo na Mtibwa Sugar waliokuwa wakicheza pasi fupi fupi.

Kiungo Thaban Kamusoko na mshambuliaji Matheo Anthon walikaribia kufunga katika dakika za 65 na 69 baada ya mashuti yao kugonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Mtibwa.

Yanga walipata pigo dakika ya 58 baada ya nahodha wao wa mchezo wa jana Juma Abdul kutolewa nje baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Yusuph Selemani.

Hata hivyo uimara wa kipa Youth Rostand kwenye mchezo wa jana uliifanya Mtibwa Sugar kushindwa kupata ushindi wa mabao mengi baada ya kuokoa hatari dakika ya 14 , 44 na 52.

Kipigo cha jana kinakuwa cha tatu mfululizo kwa Yanga kwenye ligi baada ya awali kupoteza mbele ya Simba (1-0) na Tanzania Prisons (2-0) na kufanya mabingwa hao wa zamani kupoteza michezo minne mpaka sasa kwenye michezo 26 waliyocheza.

Aidha, kipigo hicho kinamfanya kocha Shadrack Nsajigwa kutopata ushindi tangu alipoanza kuiongoza timu hiyo baada ya aliyekuwa kocha mkuu George Lwandamina kuondoka.

Chini ya Nsajigwa, Yanga imepoteza dhidi ya Simba, Tanzania Prisons, Mtibwa na mchezo mmoja wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger (4-0) ya Algeria.

Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye michuano hiyo ya kimataifa, watashuka tena uwanjani Jumatano kucheza na Rayon Sport kwenye michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.