HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Ijumaa, 4 Mei 2018

Yanga yaenda Algeria na deni

WAKATI kikosi cha Yanga kikiondoka jana jioni kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, uongozi wa timu hiyo umesema hakuna mgomo wa wachezaji lakini yakubali kushindwa kuwalipa mishahara yao.

Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh.

Akizungumza na Nipashe akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege jana mchana, Meneja wa timu hiyo, Hafidh Saleh, alisema si kweli wachezaji wa timu hiyo wamegoma kusafiri na kuongeza kuwa kila nyota aliyetarajiwa kuondoka yuko pamoja na kikosi hicho.

"Wachezaji wote tupo nao na sasa hivi tunaelekea Airport (uwanja wa ndege), sio kweli kuwa wamegoma, kama inavyosemwa lakini ni kweli wana madai yao ya mishahara," alisema Saleh na kukataa kutaja ni miezi mingapi wanadai.

Saleh alisema kuwa viongozi wameahidi kuyafanyia kazi madai yao na hali itakaa vizuri muda si mrefu na kumtaja kocha wao mpya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mwinyi Zahera, amejumuishwa kwenye safari hiyo.

"Kocha tupo naye na tunaondoka naye leo, suala la vibali hilo siwezi kuongea lolote kwa sababu sina taarifa za kina," aliongeza meneja huyo ambaye timu yake inadhaminiwa na Kampuni ya SportPesa.

YONDANI ASIMAMISHWABodi ya Ligi Kuu Tanzania imemsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani, na kumpeleka katika Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Nchini (TFF) kutokana na kitendo cha kumtemea mate, Asante Kwasi wa Simba katika mechi ya watani wa jadi iliyochezwa Jumapili iliyopita.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu, Boniface Wambura alisema pia kikao cha Kamati ya Saa 72  imekataa malalamiko ya Yanga kutaka ipatiwe ushindi dhidi ya Mbeya City ikidai kuwa wapinzani wao walikuwa na mchezaji zaidi kwenye mechi iliyowakutanisha na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 huku pia ikiipiga faini ya Sh. 500,000 Mbeya City kutokana na vurugu za mashabiki wake.

Pia kamati hiyo imeiandikia barua Yanga kuhusu kumuonya Yondani kwa sababu kumbukumbu zinaonyesha ameshafanya matukio ya utovu wa nidhamu mara kadhaa akiwa uwanjani huku vile vile ikitoa onyo kali kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, kwa kuingia uwanjani kushangilia baada ya mchezo wa watani wa jadi kumalizika.