HOUSE OF ENTERTAINMENT


JOIN KENYASWAHILINEWS
!-- AdsAgony - Ad Display Code -->

MPYA MPYA ZA LEO

HABARI (193) Michezo (121) BURUDANI (86)

Jumatano, 6 Juni 2018

BREAKING NEWZ: BASI LAGONGA TRENI KIGOMA MJINI





  Kigoma mapema leo asubuhi hii ya Jumatano Juni 6,2018, inaelezwa kuwa Basi la Hamida Trans lenye namba za usajili T 885 DLD lililokuwa likitoka Kigoma kwenda wilaya ya Nzega mkoani Tabora limegonga treni ya mizigo (Garimoshi la mizigo) katika eneo la Gungu Mjini Kigoma.

Ripota wetu aliyekuwepo eneo la tukio na kushuhudia mandhari halisi ya jali hiyo,ameeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo alfajiri, na mpaka sasa idadi ya vifo na majeruhi bado haijafahamika.

Ripota wetu yupo eneo la tukio,hivyo tutaendelea kuwaleta habari kadiri ya zitakavyokuwa zikiingia.




 Baadhi ya Askari wa JWTZ wakiwa tayari wamefika eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa namna moja ama nyingine




 Baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia tukio la ajali hiyo wakishuhudia majeruhi wakipakizwa kwenye gari  ya Wagonjwa ya JWTZ tayari kupewa huduma ya kwanza na baadae kupelekwa hospitali kwa matibabu zaidi




Mbunge wa Kigoma mjini Mhe.Zitto Kabwe akiwa eneo la tukio la ajali akishuhudia majeruhi wakiokolewa