Mshambuliaji wa raia wa Benin Marcellin Koukpo ametua nchini usiku wa kuamkia leo tayari kujiunga na Yanga.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten ndiye aliyempokea mshambuliaji huyo ambaye kesho huenda akatambulishwa rasmi kama mchezaji wa Yanga kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama.
Marcellin mwenyewe amethibitisha kutua Yanga kupita video fupi iliyotumwa kwenye ukurasa wa Intagram wa klabu ya Yanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano/Usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema kesho atafichua majina ya wachezaji watatu ambayo tayari wamesajiliwa na Yanga.